AJIRA 26 ,000 ZA WALIMU KUTOLEWA JAN, 2014

SERIKALI imetangaza kutoa ajira mpya 26,000 za walimu kuanzia Januari mwakani, ikiwa ni mpango endelevu wa kupunguza uhaba wa walimu katika shule za msingi na sekondari nchini.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), anayeshughulikia Elimu, Kassim Majaliwa, alisema hayo juzi mjini hapa wakati akifunga kikao cha kazi cha siku tatu cha maofisa elimu wa mikoa na.halmashauri za wilaya nchini,.wanaosimamia elimu ya msingi. “Serikali inatambua uhaba wa walimu na. kila mwaka inatoa ajira mpya za walimu. Januari 2014 Serikali itatoa ajira 26,000 za walimu wapya na maelekezo mengine yatafuata,“ alisema Majaliwa.

Aliwataka maofisa elimu hao kuzingatia uwiano wa walimu wakati wa kuwapangia vituo vya kazi, badala ya kuendelea.kuwalundika maeneo ya shule za mijini pekee. Pia aliagiza walimu hao watayarishiwe mazingira mazuri hasa katika maeneo ya.pembezoni kwa kuwapatia motisha, ili.kuwajengea moyo wa kufanya kazi kwa bidii na maarifa zaidi katika vituo vyao vya kazi kwa lengo la kuwafanya.wasikimbie vituo. Licha ya kutangaza ajira hizo mpya,
Majaliwa pia alisema Serikali imetenga Sh bilioni 18 za kutengeneza madawati
yatakayosambazwa shuleni na zabuni yake inatarajiwa kutangazwa mapema
iwezekanavyo. Alisema mpango huo unatarajia kuanza mapema mwakani baada ya kumpata mzabuni, “najua kutokana na kiwango kidogo cha fedha, hatutaweza kutosheleza, lakini huu ni mwanzo.” Aliwataka maofisa hao kujenga tabia ya ufuatiliaji shuleni, ili kusimamia utunzaji wa vifaa na wakikuta uzembe ni wajibu wao kuchukua hatua ya kumaliza matatizo yaliyo chini na uwezo wao.

CHANZO: HABARI LEO 23/12/2013

Related

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2014 WATANGAZWA

Jumla ya watahiniwa 411,127 kati ya 427,609 waliofaulu mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2013 wamechaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule za Serikali..Hata hivyo, kwa mujibu wa of...

BIBI WA MIAKA 99 APATA DIPLOMA

Bibi mwenye miaka 99 aliyeacha shule akiwa high school mwaka 1932 hatimaye amemaliza diploma yake. Audrey Crabtree alikuwa amezungukwa na familia yake na marafiki zake siku ya jumatatu wakati shule y...

WALIMU WALALA JIKONI -IGUNGA

Walimu walala jikoni kwa miaka mitatu! KATIKA hali ya kusikitisha, walimu wa Shule ya Msingi Iyogelo iliyoko katika kata ya Kining’inila Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, wamekuwa wakiishi jikoni ...

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in weekRecentBLOG ZINGINE

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item